Back to top

Uzalishaji wa Pweza waongezeka wilayani  Kilwa.

08 June 2022
Share

Ufungaji wa miamba katika Bahari ya Hindi  wilayani  Kilwa mkoani Lindi ,  umeongeza  uzalishaji wa samaki aina ya Pweza na kufikia tani zaidi ya sitini, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na mkoa wa Mtwara, ambao bado uko chini katika uvuaji wa samaki hao.


Kauli hiyo imetolewa na  Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Habiba Athumani, wakati wa kutoa elimu ya ufungaji wa miamba, ili kuongeza uzalishaji wa samaki aina ya Pweza.